27 Desemba 2014 - 18:51
Historia ya ugonjwa wa UKIMWI

Licha ya wanasansi kuumiza kukosa usingizi kutafuta dawa za matibabu ya ugonjwa huu, wanganga wa jadi pia hawajabaki nyuma katika kufanya jitihada za kutafuta tiba ya ugonjwa huu, na wengine Kama babu wa Loliondo walijaribu kudai kuota dawa ya ugonjwa huu lakini haikusaidia.

Historia ya UKIMWI

UKIMWI: Upungufu wa Kinga Mwilini (kwa kifupi UKIMWI; kifupi cha Kiingereza AIDS) ni ugonjwa unaotokana na virusi inayoitwa VVU na inayoshambulia mwili kwa kuondoa nguvu zake za kupambana na maradhi.

Ugonjwa huu una majina mengi sana yasiyo rasmi ambayo yanatumiwa na waswahili miongoni mwa hayo ni:Ngoma, Umeme, Miwaya, Bendi na mengineyo

Ugonjwa huu umeua watu zaidi ya milioni 36 hasa wanaoishi Kusini mwa Afrika kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani. Kwa mwaka 2005 pekee watu milioni 3.1 wamefariki na 570,000 kati yao ni watoto.

VVU husambazwa hasa kupitia ngono isiyo salama, kuongezwa damu na sindano ya kudungwa ngozini na kwa kuhama  kutoka kwa mama kwenda kwa mwaba  wakati wa ujauzito, kuzaa au kunyonyesha,

Zingatia: Baadhi ya vimiminika vya mwili, kama vile mate na machozi, havisambazi VVU.

UKIMWI hadi hivi sasa hauna dawa maalum iliyotangazwa, ingawa kuna nchi zinazosema zimetengeneza dawa na wamesha zitumia kwa wananchi wake zinakeleta matunda bila ya kuleta madhara. Miongoni mwa nchi hizo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo imetengeneza dawa ya UKIMWI inayoitwa IMOD na wameshaifanyia majaribio kwa wagonjwa wao na kutoa taarifa kuwa imefanya kazi kwa mafanikio ya hali ya juu.

Kuna dawa za kusaidia watu wenye UKIMWI. Hizi zinaitwa dawa za kurefusha maisha. Dawa za kurefusha maisha haziwezi kutibu UKIMWI. Hii ina maana kwamba haziwezi kufanya virusi zote kuondoka mwili wa mtu. Lakini zinaweza kuwasaidia watu kupambana na virusi ya UKIMWI kwa mifumo yao ya kinga kufanya kazi vizuri zaidi. Hivyo dawa za kurefusha maisha si tiba kabili kwa virusi ya UKIMWI.

Watu wenye VVU / UKIMWI ambao kuchukua dawa za kurefusha maisha wanaweza kuishi muda mrefu, bila kupata maradhi yanayothibitisha UKIMWI.

Lakini baada ya muda mrefu, virusi vya HIV visizouawa na dawa hizo hujifunza jinsi ya kupambana nazo na hivyo zinakuwa sugu kwa dawa hizo.

Baadhi ya dawa za kuongeza nguvu kwa wagonjwa wa UKIMWI ni:

D4T (stavudine)

3TC (Lamivudine)

NVP (nevirapine)

AZT (zidovudine)

EFZ (efavirenz)

Bila dawa hizo, kwa kawaida mtu mwenye VVU anayejali mashart anaweza kuishi miaka 9-11.

Licha ya wanasansi kuumiza kukosa usingizi kutafuta dawa za matibabu ya ugonjwa huu, wanganga wa jadi pia hawajabaki nyuma katika kufanya jitihada za kutafuta tiba ya ugonjwa huu, na wengine Kama babu wa Loliondo walijaribu kudai kuota dawa ya ugonjwa huu lakini haikusaidia.

Wataalamu wanasema kwamba: Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ukimwi ulitambulika kuwa janga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.

Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.

Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford na chuo cha Leuven, nchini ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia kwa Sokwe.

Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama ya wanyamapori.

Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri maelfu ya watu nchini Cameroon.

Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.

Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani, na sasa ni janga la dunia mzima.

Siku ya UKIMWI duniani huadhimishwa tarehe 1 Desemba kila mwaka ili kueneza ufahamu wa ugonjwa wa UKIMWI unaosababishwa na uambukizi wa virusi vya UKIMWI. Ni kawaida kuwa na ukumbusho huo siku hii ili kuwajali watu ambao wamefariki kutokana na VVU / UKIMWI.

 

Njia ya muhimu ya kukabiliana na ugonjwa huu si kutangaza na kuhimiza matumizi ya Condom, bali kuhimiza watu kijilinda na kujijali na kuchunga maadili na kukataza matangazo na vitu vinavyopelekea maambukizi na ushawishi wa ngono.

Tags